Kwa matokeo hayo, Yanga inatolewa kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki iliyopita, bao pekee la kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa Guinea, Yakhouba Keita aliyesaidiwa na Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere, hadi mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Wakati refa Yakhouba Keita anajiandaa kupuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo huo, Awady Said akaifungia MC Alger bao la nne akitumia makosa ya mabeki wa Yanga, Kevin Yondan na Hassan Kessy kuchanganyana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |