• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi Kuu ya Uingereza-EPL: Manchester United yaitwanga Chelsea, Liverpool yatoka kifua mbele

    (GMT+08:00) 2017-04-17 08:48:43
    Katika mechi iliyochezwa Old Trafford jijini Manchester, wenyeji Manchester United wamewatandika vinara wa ligi hiyo Chelsea magoli 2-0 na kupata uhai kuweza kumaliza ligi hiyo wakiwa katika nafasi 4 bora huku wakiacha wazi mbio za ubingwa.

    Kwa ushindi huo, Man U sasa iko kwenye nafasi ya 5 ya msimamo wa ligi hiyo wakiwa pointi 4 nyuma ya Manchester City.

    Chelsea bado wanaongoza ligi hiyo wakiwa na tofauti ya pointi 4 dhidi ya Tottenham ambayo inashikilia nafasi ya pili.

    Kwenye mechi iliyochezwa huko The Hawthorns, bao la dakika ya 46 la Roberto Firmino limewapa Loverpool ushindi dhidi ya Wet Bromwich Albion na kupaa hadi nafasi ya 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako