• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GDP ya China yaongezeka kwa asilimia 6.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-04-17 18:22:33

    Idara ya Takwimu ya China imetangaza kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, pato la taifa la China GDP liliongezeka kwa asilimia 6.9, na kudumisha mwelekeo mzuri wa kupata maendeleo kwa hatua madhubuti na utulivu katika nusu ya pili ya mwaka huu, vigezo muhimu vya uchumi ni vizuri zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

    Takwimu hizo zimeonesha kuwa, GDP ya China katika robo ya kwanza ya mwaka huu iliongezeka na kuwa asilimia 6.9 kuliko mwaka jana wakati kama huu, hili ni ongezeko la asilimia 0.2 kuliko mwaka jana. Thamani ya ongezeko la viwanda vyenye mapato ya zaidi ya Yuan milioni 20 kwa mwaka imeongezeka kwa kasi zaidi na kufikia asilimia 6.8, hali ambayo inahimiza maendeleo ya uchumi. Msemaji wa Idara ya Takwimu ya China Bw. Mao Shengyong anasema:

    "Kutokana na hali ya jumla, katika robo ya kwanza mwaka huu, uchumi wa China umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, kasi ya ongezeko la uchumi imefufuka, mageuzi ya kimuundo yanahimizwa, hatua ya maendeleo ya uvumbuzi inaharakishwa, maisha ya wananchi yanazidi kuboreshwa, maendeleo ya uchumi yameonesha mwelekeo mzuri. Lakini wakati huo huo tunapaswa kuzingatia kuwa, hali ya mazingira ya kimataifa bado ina utatanishi, mikwaruzano ya kimuundo nchini China ni mikubwa, juhudi zaidi zinahitajika katika kudumisha mwelekeo huo mzuri."

    Kutokana na muundo wa viwanda vya aina mbalimbali, viwanda vya aina ya pili vinavyohusisha na madini, utengenezaji, nishati ya umeme, gesi, maji na utoaji wa bidhaa mbalimbali, pamoja na ujenzi vimechangia zaidi kwenye ongezeko hilo la uchumi. Katika robo ya kwanza, viwanda hivyo vilichangia asilimia 36.1 ya ongezeko la GDP, hususan mwezi Januari hadi Februari, ongezeko la faida za viwanda vyenye mapato ya zaidi ya yuan milioni 20 kwa mwaka lilifikia asilimia 31.5, uzalishaji wa viwanda unazidi kuongezeka, na kuchangia sana ongezeko la uchumi kote nchini.

    Kati ya uwekezaji, matumizi na uuzaji bidhaa kwa nje ambayo ni misukumo ya jadi ya ongezeko la uchumi, matumizi yanaonesha umuhimu mkubwa zaidi, na yalichangia asilimia 77.2 ya ongezeko la uchumi katika robo ya kwanza mwaka huu, na kuonesha mwelekeo wa kuzidi kuongezeka. Bw. Mao Shengyong anasema:

    "Mapato ya wananchi yaliongezeka kwa asilimia 7.0, hili ni ongezeko la asilimia 0.5 kuliko mwaka jana wakati kama huu, huu ni msingi na uhakikisho kwa ongezeko la matumizi ya fedha. Mbali na hayo muundo wa matumizi ya fedha ya wananchi pia unabadilika, na uanzishaji wa biashara pia umeleta njia nyingi mpya ya matumizi ya fedha."

    Takwimu pia zimeonesha kuwa, uwekezaji katika uendelezaji wa mali zisizohamishika nchini China ilifikia RMB yuan trilioni 1.9, hili ni ongezeko la asilimia 9.1 kuliko mwaka jana wakati kama huu. Bw. Mao Shengyong ameeleza kama serikali itachukua hatua za kudhibiti, inapaswa kuendelea kufanya usimamizi katika sekta hiyo. Pia ameeleza kuwa duru mpya ya hatua za marekebisho na udhibiti wa sekta ya mali isiyohamishika zilianza kutekelezwa tarehe 17 Machi, athari mbalimbali zitaonekana baada ya mwezi Aprili, na hata muda mrefu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako