• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutekeleza mageuzi ya hati ya ukazi wa kudumu kwa wageni

    (GMT+08:00) 2017-04-17 18:46:46

    Mpango uliotolewa na Wizara ya usalama wa umma ya China unaonyesha kuwa, mageuzi ya kurahisisha hati ya ukazi wa kudumu kwa wageni yameanza kutekelezwa na yatakamilika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

    Habari zinasema, hati ya ukazi wa kudumu kwa wageni itabadilisha jina kuwa kitambulisho cha ukazi wa kudumu kwa wageni, na kitatumia kigezo cha teknolojia cha kitambulisho cha uraia wa China ili kiweze kutambuliwa katika mashine ya kusoma kitambulisho cha uraia wa China. Pia mfumo wa upashanaji wa habari wa reli, shirika la ndege, bima, hoteli na benki utaboreshwa ili habari za wageni wenye hati hiyo zitumike katika idara mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako