• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Mashirika ya biashara Rwanda kutafuta soko nchini Morocco

    (GMT+08:00) 2017-04-17 18:52:44

    Mashirika ya biashara ya sekta binafsi kutoka Rwanda yana mpango wa kufanya ziara nchini Morocco kwa lengo la kusaka fursa za uwekezaji .

    Mwenyekiti wa sekta binafsi nchini Rwanda Geofrey Kamanzi amesema ziara hiyo itajumuisha wafanyibiashara wa sekta za kawi,Fedha,uchukuzi,mawasiliano na ujenzi.

    Kwa mujibu wa Kamanzi,ziara hii ni mpango wa makubaliano ya nchi hizo mbili ya kuimarisha ushirikiano wa biashara.

    Kampuni kadhaa za Morocco zimeanza biashara na Rwanda baada ya ziara ya wajumbe 100 mwaka jana kwenye kongamano la biashara la Afrika.

    Nchi hizi mbili zimetia sahihi mikataba 23 ya biashara.

    Serikali za nchi hizi mbili zinataka kuvumbua biashara mpya na kuondoa vikwazo ili kuvutia wawekezaji zaidi kutoka nchi za ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako