• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya watawala mbio za Boston Marathon

    (GMT+08:00) 2017-04-18 09:05:46

    Wanariadha wa Kenya wameendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi yao na Afrika Mashariki kwa kushinda mashindano ya mbio ya Boston. Kwa upande wa wanaume, Geoffrey Kirui aliongeza kasi ikiwa imesalia maili nne hatua iliomfanya kufanikiwa na kushinda mbio hizo upande wa wanaume kwa muda wa saa 2 dakika 9 na sekunde 36.

    Raia wa Marekani Galen Rupp alimaliza wa pili sekunde 21 nyuma ya Kirui.

    Kwa upande wa akina dada, Edna Kiplagat alimaliza katika muda wa saa 2 dakika 21 na sekunde 53 ikiwa na mara yake ya kwanza kushiriki mbio hizo. Rose Chelimo pia wa Kenya aliyechukua uraia wa taifa la Bahrain alimaliza wa pili huku Mmarekani Jordan Hasay akiwa wa tatu. Bingwa mtetezi wa mbio hizo kutoka Ethiopia Atsede Baysa wa Ethiopia hakuweza kumaliza miongoni mwa wanariadha 10 bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako