• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtu aliyeshughulikia ujenzi wa mfereji kwa miaka 36

    (GMT+08:00) 2017-04-18 17:50:15

    Miaka 36 wenye siku 13,140 ni muda wa kutosha kwa watu wengi kukamilisha mambo mengi, lakini mwanakijiji anayeitwa Huang Dafa wa kijiji cha Mshikamano kilichoko Wilaya ya wakabila wa Gelao kwenye eneo la Bozhou mjini Zunyi, alishughulikia jambo moja tu, kuchimba mfereji wa maji wenye urefu wa mita elfu 10 kwenye mlima wenye kimo cha mita 300.

    Wakati wa majira ya Spring ni wakati wa kulima mashambani, wanakijiji wa Mshikamano walikuwa wakifanya kazi katika motomoto mashambani. Mwanakijiji Xu guotai alikuwa akivuta maji kutoka kwenye dimbwi la maji ili kumwagilia mashamba ya mpunga unaochipua. Xu Guotai anasema:

    "Napanga kulima mpunga na kulisha samaki, na mwaka huu kiasi kitakachovuliwa cha samaki kinatazamiwa kufikia kilogramu 1000.

    Maisha hayo mazuri hayakutarajiwa na Xu Guotai. Kabla ya mwaka 1959, umaskini lilikuwa ni tatizo lililowakabili wanakijiji wote. Chanzo kikubwa cha umaskini kilikuwa ni ukosefu wa maji. Mapigano kati ya wanakijiji kugombea maji yalitokea mara kwa mara. Wakati huo, kijana Huang Dafa aliyechaguliwa kuwa mkuu wa kijiji hicho aliamua kuongoza wanakijiji wenzake kubadilisha hali hii, na kuanza kujenga mfereji wa maji. Lakini baada ya juhudi za miongo kadhaa, kutokana na ukosefu wa teknolojia, mfereji uliharibiwa na mafuriko. Wanakijiji hawakuunga mkono tena ujenzi wa mfereji.

    Hata hivyo Huang Dafa hakukata tamaa, wakati alipokuwa na umri wa miaka 53 alitumwa katika Kituo cha maji na umeme, alijifunza elimu nyingi kuhusu teknolojia ya ujenzi wa mifereji kwa miaka mitatu. Alirudi kwenye kijiji cha Mshikamano alipokuwa na umri wa miaka 56, akiwa mkuu wa kijiji alitaka kuwaongoza wanakijiji wenzake kujenga mfereji kwa mara ya pili. Ingawa miongo kadhaa ilikuwa imepita, bado ilikuwa vigumu kujenga mfereji. Mwanakijiji aliyeshughulikia ujenzi huo Wang Zhengming anasema:

    "Mawe, mchanga na saruji iliyotumiwa kujenga mfereji vilibebwa na watu, uzito wa mawe hayo ulifikia kati ya kilo 400 hadi 500. Wakati huo katibu Huang alikuwa amezeeka lakini pia alibeba baruti za kuvunjia mawe."

    Baada ya juhudi za miaka matatu, ujenzi wa mfereji ulikamilia, na maji yalifika vijijini. Kijiji cha Mshikamano kimebadilika kutokana na maji, wanakijiji hawakuwa na wasiwasi tena wa chakula, na wameanza kuanzisha biashara ya kilimo na ufugaji. Watoto wao pia wanafanya bidii kusoma shuleni, na wanafunzi zaidi ya 30 kutoka kijiji hicho wamejiunga na vyuo vikuu . Bw Huang Dafa anasema:

    "Maji yamepatikana, sasa tunataka maisha bora."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako