• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • BD yamfungia mcheza kikapu wa DB Young Stars mwaka mmoja

  (GMT+08:00) 2017-04-19 09:23:31
  Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya DB Young Stars, Joseph Kiminsa amefungiwa kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na mchezo huo baada ya kusaini timu mbili zinazoshiriki ligi ya kikapu mkoa wa Dar es salaam (RBA).

  Pamoja na kufungiwa mchezaji huyo, timu yake imenyang'anywa ushindi na kupewa timu ya jogoo kutokana na kosa hilo. Jogoo ilipeleka malalamiko kwenye chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam (BD) ambao ni wasimamizi wa ligi ya RBA, kuwa Joseph ni mchezaji wao na wanashangaa kuichezea DB Young Stars.

  Mkurugenzi wa ufundi wa chama cha mpira wa kikapu Haleluta Kavambi amethibitisha kufungiwa kwa mchezaji huyo na kusema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa wachezaji wote wanaoshiriki ligi ya RBA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako