• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya na Malawi hakuna mbabe

  (GMT+08:00) 2017-04-19 09:24:27
  Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars na Timu ya Taifa ya Malawi Frames zimetoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

  Timu zote zilionekana kutoshana nguvu katika kila idara, ingawa kidogo mchezo wa Flames ya Malawi ulionekana kuwa juu kuliko wa Harambee. Kenya ilitumia mchuano huu kujaribu bahati yake ya nyumbani kwa mashindano ya Bara Afrika ya CHAN yatakayoandaliwa nchini humo Januari 11 hadi Februari 2 mwaka 2018.

  Kenya na Malawi zilitumia mchuano huu kujipiga msasa kwa mashindano ya Bara Afrika ya wachezaji wanaocheza soka katika mataifa yao almaarufu CHAN. Mechi hii haikuwa katika ratiba ya FIFA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako