• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na makamu mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-04-19 10:56:14

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alikutana na makamu mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bi. Federica Mogherini ambaye pia ni ofisa mwandamizi wa Umoja huo anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama.

    Bw. Li Keqiang amesema katika mazingira ya sasa ya kimataifa yenye utatanishi, China na Ulaya zinatakiwa kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa, kushirikiana katika kulinda utulivu wa kikanda na amani ya dunia, kukabiliana na changamoto kwa pamoja, kukamilisha mfumo wa usimamizi wa kimataifa na kuhimiza utandawazi wa kiuchumi na biashara huria. Amesema China itaunga mkono mafungamano ya Ulaya na kutaka kupanua ushirikiano na Ulaya katika pande mbalimbali.

    Kwa upande wake Bi. Mogherini amesema pande hizo mbili zinabeba majukumu makubwa ya kimataifa, na umoja huo unapenda kuimarisha ushirikiano na China, na kushughulika mikwaruzano kati ya pande mbili kwa hatua mwafaka. Pia anatarajia kwamba mkutano wa 19 kati ya viongozi wa pande hizo mbili utapata mafanikio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako