• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa tani 2,600 za mchele kwa Namibia

    (GMT+08:00) 2017-04-19 18:03:05

    China imekubali kutoa msaada wa tani 2,600 za mchele kwa Nambia ndani ya mwaka huu katika hafla iliyofanyika jana mjini Windhoek, Namibia na kuhudhuriwa na balozi mdogowa China nchini Namibia Bw. Li Nan na katibu wa kudumu wa ofisi ya waziri mkuu wa Namibia Bi. Nangula Mbako.

    Bw. Li Nan amesema, ukame uliodumu kwa miaka kadhaa imewaathiri wanamibia laki 6, na usalama wa nafaka unakabiliana na tishio kubwa. Amesema China itaendelea kutoa msaada wa nafaka kwa Namibia na kuunga mkono ujenzi wa miundo mbinu ya kilimo nchini humo.

    Kwa upande wake, Bi. Mbako ameishukuru serikali ya China kwa msaada wake. Amesema uungaji mkono na msaada wa kiufundi kutoka serikali ya China umeongeza imani ya Namibia, na ushirikiano wa kilimo kati ya nchi hizo mbili utapata maendeleo makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako