• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania kuboresha majukwaa na bandari kwenye maziwa makubwa matatu

  (GMT+08:00) 2017-04-20 10:07:38

  Tanzania inapanga kuyafanyia ukarabati majukwaa na bandari kwenye maziwa Viktoria, Tanganyika na Nyasa kwa mwaka ujao wa fedha, ili kuboresha usafiri kwenye maziwa hayo.

  Naibu waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Bw Edwin Ngonyani amesema tayari mamlaka ya bandari ya Tanzania TPA imeandaa mpango wa utekelezaji, kwa kushirikiana na wakala wa usimamizi wa barabara TANROADS kufanya upimaji wa kijiografia. Mpango huo utaanza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka huu.

  Pia amesema serikali itaanza kazi kubwa ya kuboresha bandari za Tanga na Mtwara pamoja, na kuweka vifaa kwenye maziwa yote ili kuboresha ufanisi wa kiutendaji kwenye bandari hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako