• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpango wa Elimu ya "Ukanda mmoja, Njia moja" wahimiza ushirikiano wa elimu kati ya nchi zilizoko katika eneo hilo

  (GMT+08:00) 2017-04-20 20:47:21

  Habari kutoka Wizara ya Elimu ya China zimesema, tangu mwaka 2016 China ilipochapisha Mpango wa kuhimiza ujenzi wa pamoja wa elimu katika "Ukanda mmoja, Njia moja", China imesaini makubaliano ya kukubaliana shahada za elimu za nchi zilizoko kwenye eneo hilo, na kuongeza nguvu katika ushirikiano wa elimu kati ya nchi hizo.

  Hadi sasa Wizara ya Elimu ya China imesaini makubaliano ya kukubadiliana shahada na nchi na sehemu 46 duniani, na 24 kati ya nchi hizo ziko katika eneo la "Ukanda mmoja, Njia moja". Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano na mawasiliano ya kimataifa katika Wizara ya Elimu ya China Bw. Xu Tao anasema:

  "Kusainiwa kwa makubaliano hayo kuna umuhimu mkubwa kwa mawasiliano kati ya wanafunzi wa China na nchi zinazohusika, na wanafunzi watakaosoma katika nchi za nje, shahada watakazopata nazo zitakubaliwa na China, wakati huo huo shahada watakazopata wanafunzi wa nchi hizo ambao watasoma nchini China, pia zitakubaliwa na serikali za nchi hizo. Mawasiliano ya watu hususan wanafunzi ni kazi kuu kwa idara ya ushirikiano ya kimataifa, na makubaliano hayo yanahimiza mawasiliano hayo."

  Takwimu zimeonesha kuwa, hadi kufikia mwaka 2016 vyuo vikuu vya China vimeanzisha ofisi 4 na miradi 98 ya elimu nje ya China ambavyo vinaenea katika nchi na sehemu 14 duniani, na mingi kati yake iko katika eneo la "Ukanda mmoja, Njia moja". Masomo yanayoanzishwa ni pamoja na matibabu na dawa za kichina, usimamizi wa viwanda na biashara, sheria, usimamizi wa fedha, pamoja na uwekezaji na uchangishaji wa fedha.

  Bw. Xu Tao ameeleza kuwa, Wizara ya Elimu itahimiza ushirikiano kati ya vyuo vikuu na viwanda vya China kwa kufuata mahitaji ya kimkakati ya taifa, ili kusukuma mbele maandalizi na ushirikiano ya wataalam. Anasema:

  "Kwa mfano wakati China inapofanya ushirikiano na Kenya kwenye ujenzi wa mradi wa reli ya mwendo kasi, serikali ya Kenya ilitumai China kuwasaidia kutoa mafunzo kwa wataalamu wa teknolojia ya reli ya mwendo kasi ambao wana shahada za vyuo vikuu. Chuo Kikuu cha mawasiliano ya Beijing kilipokea jukumu hilo na kuwasaidia kutoka mafunzo kwa wataalamu wengi. Miradi kama hiyo ni mingi sana kote nchini na inalingana na lengo la mpango wa ushirikiano wa elimu wa 'Ukanda mmoja, Njia moja'".

  Naibu waziri wa Elimu Bw. Tian Xuejun ameeleza kuwa, kwa mujibu wa makubaliano hayo ya ushirikiano, Wizara ya Elimu itatoa mafunzo kwa wataalamu, kuhimiza mawasiliano ya watu ili kupata maendeleo ya pamoja. Anasema:

  "Wizara ya Elimu itatoa misaada katika sekta za uongozaji, mawasiliano ya wanafunzi, uanzishaji wa shule nje ya China, utafiti kuhusu nchi na sehemu, mawasiliano ya utamaduni, ujenzi wa uwezo kwa sehemu iliyosaini makubaliano hayo nchini China, ili kuongoza na kuhimiza mikoa na miji kuonesha umaalumu wao na kuhimiza utekelezaji wa mpango wa elimu wa 'Ukanda mmoja, Njia moja'".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako