• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KRC Genk yaondolewa na Celta Vigo michuano ya Europa League

  (GMT+08:00) 2017-04-21 08:57:23

  Nayo timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Celta Vigo katika uwanja wake wa nyumbani wa Luminus Arena kwenye michuano hiyo ya Europa League. Katika mchezo huo KRC Genk walikuwa na mtihani wa kuvunja rekodi nzito ya Celta Vigo ambapo katika historia hawajawahi kufungwa na timu za Ubelgiji kwenye mashindano ya Europa League licha ya kuwa msimu huu ndio mara ya kwanza kwa Genk na Celta Vigo kukutana. Hata hivyo Genk waliondolewa na Celta Vigo katika hatua hiyo kwa jumla ya magoli 4-3, hiyo ni baada ya kutoka sare ya 1-1 kwa goli lililofungwa na Trossard dakika 67 baada ya Sisto kuifungia Celta Vigo goli la uongozi dakika ya 63. Lakini Genk walifungwa magoli 3-2 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Balaidos.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako