• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tottenham na Chelsea zatawala kwenye kikosi cha mwaka cha PFA

  (GMT+08:00) 2017-04-21 08:57:41

  Chama cha soka ya kulipwa nchini Uingereza (PFA) kimetangaza kikosi chake cha mwaka huku wachezaji wa Tottenham na Chelsea wakijaza nafasi nane kati ya nafasi 11.

  Kikosi hicho, ambacho kilipigiwa kura na vilabu vyote 92 vya Ligi ya Soka nchini Uingereza na vilabu vinane vya Ligi Kuu ya Wanawake, kina wachezaji watano ambao walikuwepo ndani ya timu ya msimu wa 2015-16.

  Mlinda mlango wa Manchester United, David de Gea, kiungo wa Chelsea N'Golo Kante, na wachezaji watatu wa Spurs: Danny Rose, Dele Alli, na Harry Kane wote wamejumuishwa katika kikosi cha mwisho kwa msimu wa pili mfululizo.

  Kikosi bora cha msimu huu katika Ligi ya Daraja la Pili pia kimetangazwa ambapo wachezaji wanne wa klabu iliyopandishwa daraja hadi Ligi Kuu ya England, Brighton wakiwa kwenye kikosi hicho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako