• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi nchini Uingereza yawataka mashabiki kuchukua tahadhari kwenye Marathon ya London

  (GMT+08:00) 2017-04-21 08:58:11

  Idara ya polisi nchini Uingereza imeonya mamilioni ya mashabiki wa mbio za Marathon ya London siku ya Jumapili 'kuchunga mabegi' yao dhidi ya wadukuzi na wezi.

  Kulingana na tovuti ya getwestlondon.co.uk, polisi wa Metropolitan pia wameshauri mashabiki jinsi ya kulinda mali zao. Baadhi ya mbinu za kuweka mali salama ni kuhakikisha vipochi na mabegi yanafungwa wakati wote. Pia mashabiki wameshauriwa kuandika nambari ya simu ya familia ili mawasiliano yawe rahisi simu ikiibiwa.

  Mashindano haya ya kila mwaka yatashuhudia mamia ya maafisa wa polisi wakiweka doria eneo lote la mbio hizo za kilomita 42 kuanzia Blackheath hadi The Mall mjini Westminster. Polisi wa usafiri pia watalinda barabara za chini ya ardhi jijini London.

  Mabingwa watetezi Eliud Kipchoge na Jemima Sumgong kutoka Kenya watakosa michuano hii ya 37. Kipchoge hakuingia kwenye mashindano hayo naye Sumgong amefungiwa baada ya kuvunja sheria kwa kutumia dawa haramu katika mashindano.

  Karibu washiriki 38, 000 wanatarajiwa kutimka katika michuano ya mwaka 2017.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako