• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya raga ya Kenya ya wachezaji chini ya miaka 20 yailaza Zimbabwe

  (GMT+08:00) 2017-04-21 08:58:31
  Timu ya Kenya imeanza mashindano ya raga ya Afrika ya wanaume wasiozidi umri wa miaka 20 ya wachezaji 15 kila upande kwa kuirarua Zimbabwe 34-24 jijini Antananarivo nchini Madagascar, Alhamisi.

  Vijana wa kocha Paul Odera, ambao walilimwa 27-26 na Zimbabwe katika michuano ya mwaka 2016 yaliyohusisha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19, waliongoza kipindi cha kwanza kwa 20-17.

  Hata hivyo, walijikuta chini 20-24 mapema katika kipindi cha pili kabla ya kujinasua kupitia miguso miwili iliyoandamana na mikwaju yake na kuingia fainali ya kombe hili linalofahamika sasa kama Barthes U/20.

  Kenya, ambayo haikuwahi kushinda mashindano ya Afrika ya U/19 yaliyoandaliwa kati ya mwaka 2007 na 2016 kabla ya umri ya washiriki kuongezwa hadi miaka 20, sasa itamenyana na mshindi kati ya mabingwa mara sita Namibia na Madagascar katika fainali hapo Aprili 23. Namibia, ambayo ilishinda michuano minne iliyopita, inapigiwa upatu mkubwa kuibwaga Madagascar.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako