• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwendesha mashtaka wa Ufaransa athibitisha utambulisho wa mtu aliyefanya shambulizi nchini humo

    (GMT+08:00) 2017-04-21 19:10:08

    Mwendesha mastaka nchini Ufaransa Bw. Francois Molins amethibitisha kuwa, mtu aliyefanya shambulizi la risasi katika mtaa wa Champs Elysees mjini Paris, Ufaransa jana usiku ametambuliwa, lakini hakuweza kusema zaidi kuhusiana na hilo kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea.

    Bw. Molins amesema, wachunguzi wamekagua nyumba ya mtuhumiwa huyo na inaonekana kuwa alifanya shambulizi hilo peke yake, lakini wanaendela na uchunguzi ili kubaini kama ana wenzake au la.

    Vyombo vya habari vya Ufaransa vilimnukuu mchambuzi mmoja akisema kuwa mtu aliyefanya shambulizi hilo ni mfaransa mwenye umri wa miaka 39, alikamatwa tarehe 23 mwezi Februari mwaka huu kwa kuonesha nia ya kuua polisi, lakini aliachiwa kutokana na ukosefu wa ushahidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako