• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Benki ya KCB Kenya kuanza mpango wa kustaafisha wafanyakazi kwa hiari

  (GMT+08:00) 2017-04-21 19:24:44

  Benki ya serikali nchini Kenya KCB imetangaza kwamba itaanza mpango wa kuwalipa wafanyakazi wake wanaotaka kustaafu mapema kwa hiari, hii ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuokoa shilingi bilioni 2 kila mwaka.

  Mpango wa benki hiyo wa kupunguza wafanya kazi unatokana na kwamba baadhi ya huduma zake zinaweza kupatikana kwa mtandao na hivyo haitahitaji wafanyakazi.

  Mkurungezi wa benki hiyo Joshua Oigara amesema mwanzoni mwa mwaka 2016 waliwekeza bilioni 2.5 kwenye teknolojia ili kurahisisha oparesheni zake na kukata gharama.

  Wafanyakazi wanaostaafu mapema chini ya mpango huo watapewa mafao yao yote kulingana na sheria na familia zao kupata bima ya afya kwa mwaka mzima.

  Manufaa mengine kwa wataostaafu mapema ni pamoja na kulipiwa mikopo yao kwa asilimia 25.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako