• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vurugu nchini DR Congo zalazimisha zaidi ya wacongo 11,000 kukimbilia katika Angola

    (GMT+08:00) 2017-04-22 17:32:16

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kuwa vurugu inayotokea katika majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imelazimisha zaidi ya wakimbizi 11,000 kutafuta usalama nchini Angola.

    Polisi, maafisa wa kijeshi na raia walishambuliwa na makundi ya wanamgambo, na kusababisha baadhi ya wazazi kupeleka watoto wao kuvuka mpaka, wakihofia kuajiriwa katika makundi hayo kama wangeendelea kubaki DRC.

    Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) hali ni mbaya miongoni mwa watoto, wengi wamewasili wakiwa na utapiamlo na kuhara, homa na malaria.

    UNHCR kwa sasa inaratibu wakimbizi kushirikiana na serikali, serikali za mitaa na washirika wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako