• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zoezi la kupiga kura laanza kwenye uchaguzi wa rais nchini Ufaransa

    (GMT+08:00) 2017-04-23 16:48:20

    Wapiga kura nchini Ufaransa wameanza kupiga kura leo kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais ambao utaangalia hatma ya nchi hiyo.

    Kura hizo zitapunguza orodha ya wagombea 11 hadi kufikia wawili kwa ajili ya kuwania uchaguzi mkuu wa Mei 7.

    Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi kwa saa za huko na zoezi hilo litaendelea kwa takriban saa 12 huku katika miji mikubwa vituo vikifungwa saa mbili usiku. Wapiga kura wapatao milioni 47 nchini Ufaransa wataamua mgombea yupi wa kumuunga mkono. Kati ya wagombea 11, wanne wanaongoza katika uchaguzi uliopita, ambao ni mliberali wa kati waziri wa zamani wa uchumi Emmanuel Macron, mzalendo anayeegemea upande wa kulia Marine Lew Pen, mhafidhina wa mrengo wa kulia Francois Fillon na mzalendo anayeegemea upande wa kushoto Jean-Luc Melenchon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako