• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi wa Kenya wawaua wapiganaji 52 wa kundi la Al-Shaabab

    (GMT+08:00) 2017-04-23 18:27:44

    Askari wa Kenya wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM wamewaua wapiganaji 52 wa kundi la Al-Shabaab.

    Msemaji wa jeshi la ulinzi la Kenya Kanali Joseph Owuoth amesema askari hawa pia waliharibu kambi ya kundi la Al-Shaabab iliyo katika jimbo la Lower Jubba kusini mwa Somalia, na kukatama silaha na risasi nyingi. Pia amesema mapambano dhidi ya kundi la Al-Shaabab yataendelea mpaka wapiganaji wote waangamizwe.

    Kundi la Al-Shaabab lenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda limeanzisha mashambulizi mengi nchini Somalia na nchi jirani katika miaka ya hivi karibuni. Jeshi la Umoja wa Afrika na kikosi cha usalama cha Somalia navyo vimeanzisha operesheni mbalimbali ili kuliangamiza kundi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako