• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa Uganda waliosoma nchini China na wajumbe wa makampuni ya China nchini Uganda wafanya mkutano

    (GMT+08:00) 2017-04-24 19:14:52

    Wanafunzi karibu 100 wa Uganda waliorejea baada ya kumaliza masomo yao nchini China na wajumbe wa makampuni ya China nchini Uganda wamekutana jana katika ofisi za ubalozi wa China nchini Uganda.

    Waziri wa elimu ya juu wa Uganda Bw. John Muyingo ameishukuru serikali ya China kwa ushirikiano wa kirafiki katika mambo ya elimu, na kusema, nchi hiyo inajitahidi kutekeleza kikamilifu "mpango wa muda mrefu wa mwaka 2040", na serikali inachukua nguvukazi kuwa injini muhimu ya maendeleo ya nchi.

    Balozi wa China nchini Uganda Bw. Zheng Zhuqiang amesema, katika miaka ya hivi karibuni serikali ya China inatoa msaada wa masomo kwa wanafunzi 60 wa Uganda kila mwaka ili waweze kusomea nchini China, na mwaka jana wanafunzi wapatao 400 walikwenda kusoma nchini China. Wanafunzi hao wakitumia ujuzi wao wataongeza nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi yao. Anatarajia makampuni ya China na wanafunzi wa Uganda wataanzisha utaratibu mzuri wa kufanya mawasiliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako