• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Lionel Messi ajitapa kwa mechi yao dhidi ya Real Madrid

  (GMT+08:00) 2017-04-25 08:07:28

  Juzi usiku FC Barcelona walikuwa katika uwanja wa wapinzani wao Real Madrid kucheza mchezo wao wa marudiano wa Ligi Kuu Hispania, katika mchezo huo FC Barcelona walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Real Madrid.

  Magoli ya FC Barcelona yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga magoli mawili na Ivan Rakitic, hivyo kufanikiwa kuondoka na point tatu dhidi ya wapinzani wao wa jadi na kufufua matumaini ya kuwania LaLiga ambalo kama wangepoteza mchezo huo wangekuwa katika nafasi finyu zaidi ya kutwaa taji hilo.

  Jana mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona Lionel Messi alijitapa juu ya mechi hiyo akisema walikwenda Bernabeu kuhakikisha wanapata ushindi na kurudisha nafasi yao ya kupigania Ubingwa wa La Liga hata hivyo amesisitiza kuwa bado wana safari ndefu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako