• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika Kusini zaanzisha ushirikiano wa maeneo ya sayansi na teknolojia

    (GMT+08:00) 2017-04-25 10:47:15

    China na Afrika Kusini zimezindua rasmi ushirikiano wa maeneo ya sayansi na teknolojia, ikiwa ni juhudi za kuimarisha ushirikiano wa pande mbili wa sayansi na teknolojia.

    Akizungumza kwenye uzinduzi huo, naibu waziri mkuu wa China Bibi Liu Yandong amesema, baada ya China na Afrika Kusini kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 20 iliyopita, nchi hizo zimepata maendeleo ya kasi katika ushirikiano wa sayansi na teknolojia. Amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika ushirikiano wa sekta za baiolojia, habari, uchimbaji madini, mionzi ya laser na nyingine, ambayo yamefanya sayansi na teknolojia ziwe kipaumbele katika ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Bibi Liu Yandong ameongeza kuwa, kuimarisha ushirikiano huo kutatia uhai mpya kwenye ushirikiano wa sayansi na tenkolojia kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako