• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Marekani zahimizwa kushirikiana kuleta uwiano katika biashara yao

  (GMT+08:00) 2017-04-25 18:06:56

  Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai ametoa wito kwa nchi hizo kufanya juhudi kwa pamoja ili kutimiza uwiano katika biashara yao.

  Akizungumza kwenye kongamano la ushirikiano wa kimataifa wa fedha na miundombinu la mwaka 2017 lililofanyika jana huko New York, Bw. Cui amesema, biashara kati ya nchi hizo mbili haiwezi kuepuka migogoro katika maendeleo ya kasi ya uhusiano wa uchumi na biashara, na utatuzi wake unahitaji juhudi za pande hizo mbili.

  Bw. Cui pia amesema, China inafahamu mahitaji ya wadau wa viwanda na biashara wa Marekani, kwa hiyo inafanya juhudi kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini China, ili kutoa mazingira ya ushindani yenye usawa kwa makampuni ya China na Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako