• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la "Ukanda moja na Njia moja" lafuatiliwa sana barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-04-26 18:15:22

    Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mkakati na Uhusiano wa Kidiplomasia ya Ethiopia Sebhat Nega amesema pendekezo la "Ukanda moja na Njia moja" limetoa jukwaa muhimu kwa kutimiza maendeleo ya pamoja kwa Asia, Ulaya na Afrika na kutoa fursa mpya za uwekezaji, biashara na ajira.

    Bw. Sebhat amesema hayo alipohudhuria kongamano la mtazamo wa Afrika lililofanywa na ubalozi wa China nchini Ethiopia na Taasisi hiyoa. Amesema pendekezo hilo pia litaimarisha mawasiliano kati ya nchi kwenye ukanda huo, lakini siyo kifaa cha siasa za kijiografia kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

    Wajumbe waliohudhuria kongamano hilo walitoa maoni na mitazamo mipya kuhusu pendekezo hilo, ambapo balozi wa China nchini Ethiopia Bw. La Yifan alizitaka nchi za Afrika zijiunge na pendekezo la "Ukanda moja na njia Moja" la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako