• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpango wa China wa Ukanda Mmoja na Njia Moja utanufaisha pande zote, asema mtaalama wa sera na mikakati

  (GMT+08:00) 2017-04-28 09:44:24

  Mpango wa China wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ulioanzihswa na Rais wa China Xi Jinping, umeleta mwamko mpya wa kibiashara barani Afrika.

  Mkakati huo ni mpango mpya na mpana wa kufufua njia ya Hariri ya kale ya baharini sasa ikiwa itasaidia nchi nyingi kukua kiuchumi.

  Dkt. Robert Kagiri mkurungezi wa kituo cha mikakati na usimamizi wa sera Afrika anasema mkakati huo wa China utakuwa na manufaa ya pande zote husika.

  "Huu mpango wa Ukanda mmoja na njia moja ni muhimu sana kwa Afrika, kwa maana vile sasa china wanataka kujipanua kutokla vile walikuwa wamejifungia, sasa watafanya biashara na ulimwengu. Na Afrika ni muhimu sana kwa hiyo mpango yao. Rais wao Xi Jinping amesema anatafuta njia ambazo kuna ushindi kwa pande zote katika mambo ya biashara na ujenzi "

  Kama njia moja ya kuendelea kusukuma mbele miradi ilioko chini ya mkakati huu, China mwezi Mei itaandaa mkutano wa viongozi wa nchi na serikali kutoka nchi inakopitia njia ya Hariri ya baharini.

  Huu utakuwa mkutano wa kwanza kuhusu Ukanda mmoja na njia moja lakini sio tu nchi hizo pekee bali ni mkutano wazi kwa nchi zote.

  "Hiyo mkutano ni muhimu sana kwa sababu wataweza kuonyesha njia ambazo Aarika inaweza kuingia hiyo mkakati hata kuliko vile ilivyo sasa. Kuna nchi kama Madagascar ambazo zimeenda China kuuliza kujumuishwa kwenye mkakati huo na ukiangalia nchi kama Kenya tayari kutokana na hii reli ya kisasa, tumeingia tayari kwenye mkakati kwa maana sisi ndio tunafungua Afrika"

  Huu ni mkakati wa kihistoria wa Rais Xi Jinping wa kuwekeza mabilioni ya fedha kwenye miradi ya miundo mbinu kama vile reli, kawi na bandari kote barani Afrika, Asia na Ulaya.

  Dkt kagiri anasema mkakati huo wa China sio tu unalenga kujenga barabara na reli lakini manufaa yake yanasambaa hadi kwenye nafasi za ajira, uhamishaji wa teknolojia na ujuzi.

  Pia itakuwa ndio ufunguo wa Afrika wa kufanya biashara baina ya nchi barani humo.

  "Ukanda mmoja na njia moja inashikana na mipango ya Afrika ya kushikanisha nchi zote kwa barabara, kwa reli na kwa ndege ili ziweze kufanya biashara pamoja bali na biashara na wachina tu. Ile kitu imekuwa ikitusumbua sana Afrika ni vile hakuna njia rahisi ya kufika nchi nyingine"

  Huku sasa miradi ya Ukanda mmoja na Njia moja ikianza kutekelezwa katika nchi mbalimbali, ni wazi kwamba manifaa yake ya miaka 5 ijayo yatakuwa makubwa kwa jamii na uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako