Taarifa pia inaonyesha kuwa asilimia 62 ya matukio yaliyosababisha vifo na majeruhi yalipangwa na wapiganaji wanaopinga serikali, kiasi ambacho kimeongezeka kwa asilimia 5 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. mabomu na milipuko ya kujitoa muhanga bado ni njia kuu zinazosababisha vifo na majeruhi zaidi kwa raia.
Eneo lenye wahanga wengi zaidi ni mkoa Kabul, ukifuatiwa na mkoa wa Helmand, Kandahar na Nanagarhar. Mashambulizi mengi yaliwalenga watumishi wa serikali, wazee wa makabila na wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |