Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu Stephen O'Brien ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa mapigano katika maeneo mbalimbali nchini Syria mwezi uliopita.
Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syrtia, O'Brien amesema mashambulizi dhidi ya vituo vya afya hayakubaliki na ni lazima yasimamishwe. Aidha, O'Brien amesema bado wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali katika mji wa Khan Shaykhun mapema mwezi huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |