• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli awafukuza kazi watumishi wa umma zaidi ya 9000 wenye vyeti vya kughushi

    (GMT+08:00) 2017-04-29 17:23:44

    Rais wa Tanzania John Magufuli jana aliwafukuza kazi watumishi wa umma 9,932 waliogundulika kuwa na vyeti vya kughushi baada ya kufanyiwa uhakiki wa vyeti vyao vya shule.

    Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya kupokea ripoti juu ya uhakiki wa vyeti vya shule vya watumishi hao wa umma. Rais Magufuli ameamuru mshahara wa mwezi Aprili wa watumishi hao kuzuiwa na kushtakiwa mahakamani. Aidha amemtaka waziri mkuu Kassim Majaliwa kutangaza nafasi za kazi zilizokuwa zikishikiliwa na watumishi hao wenye vyeti vya kughushi.

    Magufuli amesema msako wa vyeti feki umesaidia zoezi la serikali kutambua wafanyakazi hewa na kusisitiza kuwa serikali ilikuwa ikipoteza takriban dola milioni 10 za Kimarekani kwa wafanyakazi hao hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako