• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa yazitaka pande zinazopigana Sudan Kusini kusitisha mapigano

    (GMT+08:00) 2017-04-30 19:10:22
    Umoja wa Mtaifa umesema kuwa unasumbuliwa na kuongezeka kwa vurugu na mateso ya raia nchini Sudan Kusini na kuitaka serikali na vyama vingine kusitisha mapigano nchini humo.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa bwana Stephane Dujarric amesema, Umoja huo unawataka kusitisha mapigano mara moja na kuchukua jukumu la kulinda raia na kushirikiana na umoja wa mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu kuhakikisha usalama wa kila raia na kutotokea hatari pamoja na benki ya magharibi ya mto Nile.

    Katika mkutano wa 25 wa Mamlaka ya Maendeleo ya kitaifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (IGAD) imetaka utekelezaji wa kusitisha mapigano na kuwezesha upatikanaji wa haki za kibinadamu na kufuatilia makubaliano ya amani Sudani Kusini, na kuonya kuwa kuongezeka kwa njaa na migogoro kusababisha ghasia vinadhoofisha jitihada zote za kutafuta amani nchini humo.

    Naye mwenyekiti wa Tume ya ufuatiliaji na utathmini (JMEC), Festus Mogae amesema Sudani Kusini kwa sasa inakabiliwa na mgogoro ndani ya mgogoro huku kukiwa na kupanda kwa bei kwa vitu vya msingi, vurugu na biashara kufungwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako