• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapunguza viwavi jeshi kwa asilimia sabini

    (GMT+08:00) 2017-05-01 09:13:00

    Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Bw William Ole Nasha amesema wizara yake imepeleka wataalamu wa kilimo kwenye mikoa iliyoathiriwa zaidi na viwavi jeshi na kufanikiwa kuwapunguza wadudu hao kwa asilimia 70.

    Wimbi la viwavi jeshi wenye asili ya Amerika ya kaskazini na Amerika ya Kusini wamesababisha madhara makubwa kwenye maeneo 12 nchini Tanzania. Waziri Ole Nasha amesema asilimia 30 ya eneo la Tanzania imeathiriwa na viwavi jeshi walioharibu mamia ya ekari za mahindi, huku wakulima wakilalamika kuhusu gharama kubwa za kukabiliana na wadudu hao.

    Kenya pia inapambana na viwavi jeshi ambao hadi sasa wameathiri hekta elfu 11 za mahindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako