• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mishahara ya wafanyakazi wa Kenya si sawa na hali ya maisha hivi sasa

    (GMT+08:00) 2017-05-01 19:53:43

    Mishahara ya wafanyakazi wa Kenya si sawa na hali ya maisha hivi sasa.

    Ulimwengu ukiwa unaadhimisha Siku ya wafanyikazi Gharama ya maisha imeendelea kupanda huku wafanyikazi wanaendelea kulipwa mishahara ya chini.

    Takwimu rasmi inaonyesha wafanyakazi walipata ongezeko kidogo la asilimia 0.1 la mishahara yao katika mwaka wa fedha uliokamilika Juni 30.

    Mfumuko wa bei umeathiri wale wenye kipato cha chini, ambao wanakabiliana na gharama kubwa za maisha ya asilimia 11.48 inayotokana na kupanda kwa bei za vyakula.

    Mapato halisi ya wafanyikazi imepungua kwa kasi kutoka asilimia 10.7 mwaka wa 2013 hadi asilimia 2.9 mwaka wa 2015 na hatimaye asilimia 0.1 mwaka jana, kuonyesha kudhoofika kwa uwezo wao wa ununuzi.

    kushuka kwa ukuaji wa mapato umekuja licha ya utulivu wa mfumuko wa bei, ina maana kuwa makampuni yalikosa kuongeza mishahara ya wafanyakazi katika mwaka wa fedha uliokamilika.

    Kulingana na hali ya uchumi ni kwamba mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 7.0 mwezi Juni mwaka wa 2015 hadi asilimia 5.8 mwezi Juni mwaka wa 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako