• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sportpesa: hatimaye mshindi wa jackpot ya sportpesa apatikana

    (GMT+08:00) 2017-05-02 08:52:40
    Mkenya aliyefanikiwa kubashiri kwa ufasaha matokeo ya mechi 17 mwishoni mwa wiki amejishindia jumla ya Shilingi milioni mia mbili za Kenya ambazo ni sawa na dola milioni 2.2 za Marekani.

    Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye ni mzaliwa wa Kakamega, magharibi mwa Kenya ndiye wa kwanza kujishindia kiasi kikubwa hivyo cha pesa.

    Mshindi huyo wa Mega Jackpot ya kampuni ya Sportpesa alianza kushiriki mashindano ya bahati nasibu ya kubashiri matokeo mwaka jana baada ya kutambulishwa kwa mchezo huo na nduguye.

    Mshindi huyo atatambulishwa rasmi leo katika sherehe itakayofanyika mjini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako