• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yataka raia wa eneo la Aburoc Sudan Kusini walindwe

    (GMT+08:00) 2017-05-02 09:21:56

    Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Serge Tissot, jana alitaka maelfu ya raia wanaoishi ndani na karibu ya mji wa Aburoc walindwe, kufuatia kuanza kwa mashambulizi ya serikali katika maeneo kadhaa ya Ukingo wa Magharibi na Upper Nile wiki iliyopita.

    Bw. Tissot ametaka pande zinazopambana kuwajibika kuwalinda maelfu ya raia wa Shilluk wanaoishi katika mji wa Aburoc. Amesema wananchi hao wanaishi kwa hofu, bila kujua nini kitatokea baadaye, hivyo ameitaka serikali kuheshimu makazi hayo na kuhakikisha raia hao hawalengwi kwenye mashambulizi.

    Kwa mujibu wa Bw. Tissot raia wengi wanakimbilia nchini Sudan, hata hivyo amesema haikubaliki kuona wanalazimishwa kukimbia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako