• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya: Real Madrid yaiangamiza Atletico Madrid

  (GMT+08:00) 2017-05-03 10:14:57

  Nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani ulaya imechezwa jana katika uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid kwa kuzikutanisha timu ya Real Madrid na Atletico Madrid.

  Real Madrid imeibuka na ushindi wa magoli 3-0, magoli yote yamefungwa na Christiano Ronaldo katika dakika ya 10, 73 na 89. Hii ni hat trick ya 42 kwa mchezaji huyo kufunga akiwa anachezea timu yake ya Real Madrid.

  Timu hizo zitarudiana Mei 10 katika uwanja wa Vicente Calderon Madrid. Mechi ya pili ya nusu fainali inapigwa leo kati ya AS Monaco dhidi ya Juventus.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako