• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya mkoa wa Galmudug nchini Somalia yatakiwa kumaliza tofauti kwa njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2017-05-03 17:28:59

    Umoja wa Mataifa na wenzi wa kimataifa wa Somalia wametoa wito kwa viongozi wa jimbo la Galmudug kumaliza tofauti zao kupitia mazungumzo na maafikiano.

    Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, wajumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, na Marekani wamesema kuwa majadiliano yanayolenga kutimiza maafikiano yamesitishwa. Wenzi hao wamezitaka pande zote kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga juhudi za maafikiano, na kwamba wenzi hao wako tayari kuratibu mchakato wa maafikiano kama pande hizo zitakubali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako