• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Turkana imepokea sh milioni 86.8 kwa ajili ya ukarabati wa barabara

    (GMT+08:00) 2017-05-03 19:53:15

    Kaunti ya Turkana imepokea utoaji wa pili mkubwa wa fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara kwa muda wa miezi sita, takwimu kutoka Mamlaka ya Barabara inaonyesha.

    Kwa mujibu wa takwimu, kaunti ya nyumbani ya visima vya mafuta nchini Kenya vinavyoendeshwa na kampuni ya Uingereza ya mafuta Tullow, ilipokea sh milioni 86.8 katika kipindi cha miezi sita, hivyo kuifanya kaunti ya pili baada ya Nairobi kupokea sh milioni 107.7.

    Hii ina maana kwamba kaunti ya Turkana hadi kufikia sasa imepokea sh milioni 173.6 wakati Nairobi imepokea sh milioni 215.4.

    Kulingana na mpango wa mapema wa uzalishaji wa mafuta, Tullow inatarajiwa kutumia barabara na mfumo wa reli wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Lokichar hadi bandari ya Mombasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako