• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kiwanda kipya kinatarajiwa kuanza kwa ajili ya kuunganisha pikipiki

    (GMT+08:00) 2017-05-03 19:53:40

    Kiwanda kipya kinatarajiwa kuanza kwa ajili ya kuunganisha pikipiki katika eneo la biashara Kigali, hatua hii inatarajiwa kupunguza gharama ya pikpiki nchini.

    kiwanda, cha Pikipiki Rwanda (RMC), inatarajiwa kuanza kuunganisha pikipiki mwezi huu.

    Pikipiki ndiyo njia ya usafari kwa kawaida nchini Rwanda na ni bora na gharama yake ni nafuu.

    uwekezaji wa awali katika kiwanda cha kuunganisha pikipiki ni dola milioni 1.2 lakini uwekezaji zaidi unatarajiwa kulingana na mafisa wa serikali.

    Kulingana na mkurugenzi wa kampuni hiyo McPhee Christopher, ni kwamba wanataka kukuza bidhaa zinazotengenezwa nchini Rwanda kwa kushirikisha kampuni ya ndani ya vyuma na makampuni mengine ya ndani kusambaza vifaa.

    kampuni inatarajia kujenga ajira kwa zaidi ya mafundi 100 wa ndani.

    gharama ya pikipiki ni kati ya Rwf milioni 1.2 na Rwf milioni 3, hii ni kulingana na Louis Masengesho, Meneja wa soko katika kiwanda hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako