• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi cha madaktari wa China chachangia kuboresha sekta ya afya ya Sudan

    (GMT+08:00) 2017-05-04 09:45:10

    Mamlaka za Sudan Kusini zimepongeza juhudi za China katika kuunga mkono sekta ya afya nchini humo kwa kuchangia wataalamu 15 wa sekta ya afya kwa nchi hiyo kila mwaka katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

    Tangu Sudan Kusini ipate uhuru mwaka 2011, China imetuma vikundi vitano vyenye jumla ya wahudumu wa afya 66, ambao wametoa matibabu maalum na kufanya upasuaji kwa zaidi ya wagonjwa elfu 55 wa Sudan Kusini.

    Akiongea kwenye sherehe ya kuwaaga madaktari wa China waliomaliza muda wa mwaka mmoja kutoa huduma nchini Sudan Kusini, Waziri wa afya wa nchi hiyo Bw Riek Gai Kok amesema hakuna shaka kuwa sekta ya afya ya Sudan Kusini inahitaji uungaji mkono wa China kwa sasa kuliko wakati wowote ule.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako