• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yakutaja kujiunga kwake na benki ya AIIB kama hatua muhimu ya kuondoa utengwaji kiuchumi

    (GMT+08:00) 2017-05-04 10:32:40

    Wachambuzi wa uchumi wa Sudan wamesema, ushiriki wa nchi hiyo katika Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB ni hatua muhimu ya kuondoa hali ya kutengwa kiuchumi inayoikabili nchi hiyo.

    Mchambuzi Bw. Mohamed Nayer amesema hatua hiyo imekuja wakati Sudan inakumbwa na vizuizi vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani kwa miaka 20 iliyopita.

    Ameongeza kuwa Sudan inahitaji miundombinu inayohimiza uwekezaji katika sekta mbalimbali. Nchi hiyo pia inahitaji kutumia mfuko uliotolewa na benki hiyo kwa usawa na uwiano, badala ya kufuata vigezo vya kisiasa vilivyowekwa na Benki ya Dunia na IMF.

    Mchambuzi mwingine wa nchi hiyo Bw. Adil Abdul-Khaliq pia amesisitiza umuhimu wa kutunga mpango mkubwa na kutumia fursa zenye manufaa zinazotolewa na benki ya AIIB.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako