• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Marekani asema makubaliano ya amani kati ya Palestina na Israel yaweza kufikiwa

  (GMT+08:00) 2017-05-04 19:33:13

  Rais Donald Trump wa Marekani amesema nchi yake itafanya juhudi katika kuzihimiza Israel na Palestina zifikie makubaliano ya amani, na lengo hilo linaweza kutimia.

  Rais Trump alisema hayo wakati alipozungumza kupitia televisheni pamoja na rais Mahmoud Abbas wa Palestina ambaye yuko ziarani nchini Marekani.

  Rais Trump pia amesema, nchi yoyote ikiwemo Marekani haiwezi kuzilazimisha Israel na Palestina zifikie makubaliano, na kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kufanya juhudi kutimiza lengo hilo litakalozisaidia pande hizo mbili kuishi na kustawi kwa pamoja.

  Kwa upande wake, Rais Abbas alisema kuwa, anaamini kuwa Palestina na Israel zinawezekana kufikia makubaliano ya kutatua mgogoro kati yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako