• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya TAZARA yatarajiwa kupata uhai mpya

    (GMT+08:00) 2017-05-04 20:00:02

    Wapendwa wasikilizaji, reli ya TAZARA ilijengwa kwa ajili ya kuunga mkono mapambano ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, lakini ilidorora baada ya kumalizika kwa mapambano hayo. Hivi sasa ukiwa mmoja kati ya miradi muhimu ya China ya kutoa misaada kwa nchi za nje, je hali ya reli hiyo ikoje?

    Bw. Mwanyika ambaye alikuwa dereva wa treni kwenye reli hiyo alistaafu rasmi mwaka jana baada ya kufanya kazi kwa miaka 41. Kati ya mwaka 1976 hadi mwaka 1986, Bw. Mwanyika aliendesha garimoshi katika reli hiyo kwa miaka kumi. Anasema:

    "Nilipokuwa dereva, kulikuwa na magarimoshi 12 yanafanya kazi kila siku."

    Lakini sasa idadi ya magarimoshi imepungua kuwa mawili hadi manne kwa siku. Mbali na hayo, hapo zamani mshahara wa Bw. Mwanyika ulikuwa fahari ya familia yake, lakini kuanzia mwaka jana alipostaafu hadi sasa bado hajapewa malipo.

    Kwa kweli ikilinganishwa na hali ya zamani, hali ya reli hiyo iliyofanya kazi kwa miaka 40 si nzuri sana. Kati ya mwaka 2015 hadi 2016, uchukuzi wa mizigo ya reli hiyo ilikuwa tani laki 1.3, na lakini kiasi hicho kilikuwa tani milioni 1.27 wakati wa kilele cha uchukuzi wa mizigo cha reli hiyo.

    Akizungumzia hali hiyo meneja mkuu wa Idara ya usimamizi wa Reli ya TAZARA Bw. Bruno Ching'andu ameeleza kuwa, kushuka kwa kiasi cha uchukuzi wa mizigo ni chanzo muhimu cha matatizo yanayoikabili reli hiyo. Lengo la ujenzi wa reli ya TAZARA lilikuwa kuisaidia Zambia iliyotangulia kujipatia uhuru kati ya nchi za kusini mwa Afrika kuvunja vizuizi vya usafirishaji wa madini ya shaba nje ya Zambia vilivyowekwa na serikali ya ubaguzi wa rangi ya wazungu wa Afrika Kusini. Chanzo cha bidhaa kilipungua kutokana na mabadiliko ya hali ya mapambano katika nchi hizo zilizoko kusini mwa Afrika, lakini reli hiyo haikufanyiwa marekebisho yanayolingana na hali hiyo. Anasema:

    "Tulikuwa tukichukua hatua taratibu kukabiliana na mabadiliko hayo, hali ambayo ilisababisha kushuka kwa kiasi cha uchukuzi wa reli hiyo, kupungua kwa mapato na kupungua kwa ufanisi wa uendeshaji. Mwishowe huduma zetu hazikuweza kukidhi mahitaji ya wateja, wakachagua njia nyingine za uchukuzi."

    Lakini sasa garimoshi ya reli hiyo linatoa huduma kikamilifu. magarimoshi 18 kati ya abiria yalitolewa na serikali ya China, yalianza kutumiwa katika reli ya TAZARA mwishoni mwa mwaka 2015. Bw Miao Zhong anasema:

    "Kama marafiki wenyeji wanavyosema, reli ya TAZARA isingeweza kutumika leo bila ya ushirikiano wa teknolojia ya China."

    Meneja mkuu wa Idara ya usimamizi wa reli ya TAZARA Bw. Bruno aliyeingia madarakani mwezi Aprili mwaka jana, ana mipango mingi kuhusu mustakabali wa reli hiyo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha muda wa uchukuzi wa mizigo katika safari nzima ndani ya siku tano, kupunguza kituo cha kuweka mipaka kwa kasi ya magarimoshi hadi 8, na kununua magarimoshi mengi zaidiā€¦ Lakini kwa maoni ya Bw. Miao Zhong, China itahitaji kuongeza nguvu katika utengaji wa fedha na watu, ili kuifanya reli hiyo ipate uhai mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako