• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua msimamo wa haki katika suala la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-05-04 20:44:45

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China siku zote inachukua msimamo wa haki katika suala la kutimiza Peninsuala ya Korea isiyo na silaha za nyuklia, na uendelezaji wa uhusiano kati ya China na Korea ya Kaskazini.

    Bw. Geng Shuang amesema hayo alipozungumzia makala iliyotolewa na Shirika la Korea ya Kaskazini inayoikosoa China kwa kuiwekea vikwazo Korea ya Kaskazini.

    Bw. Geng amesisitiza kuwa China inashikilia kulinda amani na utulivu katika peninsula ya Korea, na kuhimiza utatuzi wa suala hilo kwa njia ya mazungumzo. Pia China inatumai pande nyingine zinazohusika zitaweza kubeba majukumu yao, ili kuchangia katika kuleta amani na utulivu na faida za pamoja kwa wananchi wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako