• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbio za Diamond League kuanza leo Doha

  (GMT+08:00) 2017-05-05 09:04:53

  Mbio za Diamond League mwaka 2017 zinatarajiwa kutimua vumbi leo jijini Doha nchini Qatar. Mabingwa wa Olimpiki Conseslus Kipruto, Caster Semenya na Ruth Jebet ni baadhi ya wakimbiaji wanaopigiwa upatu kuanza msimu vyema hasa baada ya kutikisa mwaka 2016. Semenya anatetea taji la Doha

  Mbio za mita 3,000 za wanaume pia zinatarajiwa kuwa moto ambapo Kipruto atamenyana na Wakenya wenzake Edwin Soi, Caleb Ndiku, Thomas Longosiwa, Collins Cheboi na Ronald Kwemoi. Tishio kubwa katika kitengo hiki ambacho kimevutia washiriki 17 ni Yomif Kejelcha kutoka Ethiopia. Bingwa wa dunia Nicholas Bett na mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki, Boniface Mucheru watapeperusha bendera ya Kenya katika mbio za mita 400 kuruka viunzi. Kitengo hiki kitaleta pamoja washiriki wanane wakiwemo bingwa mara tatu wa Afrika, Louis Van Zyl wa Afrika Kusini na bingwa wa Olimpiki, Kerron Clement.

  Wakenya Eunice Sum na Margaret Nyairera wana kibarua kigumu katika mbio za mita 800 dhidi ya mabingwa wa Olimpiki, Caster Semenya (Afrika Kusini) na Genzebe Dibaba (Ethiopia). Washiriki wengine ambao pia hawawezi kupuuzwa ni Mjerumani Johanes Vetter (Ujerumani), Jakub Vadlejch (Czech), Hamish Peacock (Australia), Ryohei Arai (Japan), Kim Amb (Uswidi) na wenyeji Mohamed Ibrahim na Ahmed Magour.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako