• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la chini la bunge la Marekani lapitisha muswada wa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya

    (GMT+08:00) 2017-05-05 09:24:35

    Baraza la chini la bunge la Marekani limepitisha muswada wa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya kwa kura 419 za ndiyo na kura 1 ya hapana, na sasa unasubiri kufikishwa kwenye baraza la seneti ujadiliwe.

    Muswada huo mpya unapiga marufuku meli za Korea Kaskazini kwenye maeneo ya bahari na bandari za Marekani. Pia bidhaa za Korea Kaskazini zilizotengenezwa na nguvu kazi ya kulazimishwa haziruhusiwi kuingia kwenye soko la Marekani.

    Muswada huo pia unaitaka serikali ya Donald Trump iliarifu bunge la Marekani kama kuna haja ya kuiwekea upya Korea Kaskazini kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi ndani ya siku 90.

    Mwezi uliopita serikali ya Marekani ilisema itaimarisha vikwazo vya kiuchumi na shinikizo la kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskazini ili kuondoa silaha za nyuklia katika Penisula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako