• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Guterres atarajia kuona makubaliano yanaboresha maisha ya watu nchini Syria

    (GMT+08:00) 2017-05-05 18:53:13

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kutiwa moyo kwa kusainiwa makubaliano mapya ya Syria, na kusema hatua hiyo itakuwa muhimu katika kuboresha maisha ya Wasyria.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, makubaliano hayo yalifikiwa na nchi wadhamini zikiwemo Iran, Russia na Uturuki ili kuondoa vurugu katika maeneo muhimu nchini Syria. Aidha imesema Bw. Guterres amepongeza nia ya kusitisha matumizi ya silaha, hususan za mashambulizi ya anga, ili kuweza kupatikana misaada ya kibinadamu kwa haraka, usalama bila kizuizi chochote, na kutoa mazingira ya ufikishwaji wa misaada ya matibabu na mahitaji ya msingi ya raia.

    Jana Russia, Iran na Uturuki zilisaini makubaliano hayo huko Astana Kazakhstan ili kuwekwa maeneo manne salama nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako