• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvua kubwa yasababisha uharibifu wa Mali Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-05 19:04:44

    Mvua kubwa ambayo imeanza kunyesha maeneo kadhaa nchini Kenya imesababisha uharibifu mkubwa wa mali na barbara. Baadhi ya watu wamelalamikia mali zao kubebwa na mvua hiyo ambayo pia ilisababisha mafuriko makubwa na kutatiza shughuli za biashara.Katika eneo la bonde la ufa, usafiri na biashara zilisimama kwa saa kadhaa baada ya mvua kuanza kunyesha ghafla jana jioni. Kwenye barabara kuu ya Lamu kuelekea Mombasa madereva walilazimika kupunguza mwendo kutokana na utelezi. Baadhi ya madereva wa biashara ya usafiri wa boda boda waliozungumza na radio China Kimataifa, wameitaka serikali kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ili kupunguza matatizo wanayokumbana nayo. Aidha wanabodaboda hao wamesema biashara zao zimekatizwa kwa kiwango kikubwa .Katika eneo la Kisumu wakulima wa miwa wanadaiwa kuathirika mno baada ya kushindwa kuwasilisha mazao yao kwa viwanda vya sukari katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako