• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauritus yatarajia kuwa jukwaa la China katika kuwekeza barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-05 19:19:45

    Waziri mkuu wa Mauritus Bw. Pravind Jugnauth hivi karibuni alisema kuwa pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja limeziletea nchi nyingi fursa ya maendeleo, na kwamba Mauritus inatarajia kuimarisha ushirikiano wake na China kwa kupitia ujenzi wa Ukanda mmoja na Njia moja ili kutimiza maendeleo yake endelevu.

    Bw. Pravind alisema, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Mauritus miaka 45 iliyopita, ushirikiano kati ya pande mbili kwenye sekta mbalimbali umeendelea kwa kasi, kwani China ilifanya juhudi kubwa katika ujenzi wa miundo mbinu, fedha na tekenolojia nchini Mauritus. Ameongeza kuwa hivi sasa Mauritus inahitaji kuimarisha uvumbuzi wa teknolojia na kuongeza uwezo wa uzalishaji na ushindani, ili kutimiza maendeleo endelevu. Alisisitiza kuwa, Mauritus inaweza kuunganisha Asia na Afrika, na kutarajia kuwa mlango na jukwaa la China katika kuwekeza barani Afrika.

    Akizungumzia kuhusu utalii kati ya China na Mauritus Bw. Pravind amesema . Shirika la ndege la Mauritus litachukua hatua nyingi za kuwavutia wageni wa China, zikiwemo kutumia ndege za aina mpya za abiria na kuajiri watumishi wa ndege wanaoongea Kichina, ili kuinua ubora wa huduma kwa abiria wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako